Kilio kikuu cha Yesu, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?”, yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”, na “Imekwisha”, vilitabiriwa katika Zaburi 22 ili watu waliompinga Kristo waamini kama Yesu alikuwa Masihi. Zaburi 22 ulikuwa wimbo maarufu katika kipindi cha karne ya kwanza, kipindi ambacho Yesu alizaliwa na kufa, uliotungwa na mfalme Daudi, ulioitwa ‘zaburi ya mateso na matumaini ya mwadilifu’. Kwa hiyo Yesu aliposema maneno hayo yaliwaingia watu akilini, na kuanzia hapo imani hasa ya Ukristo ikachukua kasi hadi leo hii. Zaburi 22 inaanza na “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” na inaisha na “Imekwisha”, miongoni mwa maneno saba aliyoyasema Yesu pale msalabani Golgotha. Kwa hiyo, Zaburi 22 ni utabiri wa kifo cha Yesu.